Kamati ya Jamii · JMMBA

Bima ya Faraja.

Mpango wa Bima ya Maisha ya Vikundi kwa wanachama wote wa JMMBA. Ulinzi wa fedha kwa familia yako — msiba ukitokea, malipo yanafanyika ndani ya saa 24–48. Mara moja kwa mwaka. Hakuna kuchangishana kila wakati.

🏦 CRDB Bank & Sanlam Life Tanzania
⏱ Malipo: ~wiki moja (saa 48 za CRDB, inategemea hati)
49
Familia zilizojiunga 2026-2027
10M
Fao la juu (AMANI) kwa mwanachama (TZS)
~1 wiki
Muda wa kawaida wa malipo (CRDB wanasema saa 48, inategemea haraka ya hati)
6,000
Ada ya AMANI kwa mwezi (72,000/mwaka)
Kwa nini bima ya vikundi?

Hakuna tena mchango wa haraka haraka kila msiba.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, JMMBA ilikusanya jumla ya TSh 25,167,467 kama rambirambi kwa familia za wanachama waliopatwa na misiba kumi.

Kwa kulinganisha, kama JMMBA ingekuwa imejiunga na Bima ya Vikundi tangu mwanzo, tungekuwa tumepokea zaidi ya TSh 100,000,000 kwa ajili ya kuwafariji wafiwa. Hiyo ni tofauti ya mara nne — hata ukizingatia kwamba malipo yanaweza kuchukua karibu wiki moja badala ya saa 48 zinazotangazwa.

Malipo ya mara moja kwa mwaka
Hakuna kuchangishana kila mara msiba ukitokea.
Ulinzi wa familia nzima
Mwanachama, mwenza, watoto hadi wanne — wote wana kinga.
Malipo yanakuja — bila kuombaomba
CRDB wanasema saa 24–48, lakini kwa uzoefu wetu inachukua karibu wiki moja kulingana na haraka ya kupata hati kutoka kwa wafiwa. Bado ni bora zaidi kuliko mchakato wa kawaida wa kukusanya michango.
Msaada wa elimu kwa watoto
Fao la elimu la 600,000 TZS kwa watoto wa marehemu — hata kama hana mtoto.
Chagua mpango wako

Vifurushi vinne — tofauti za ada na mafao.

JMMBA imechagua mpango wa AMANI kama mpango mkuu wa kikundi. Wanachama wanaopenda kiwango kingine wanaweza kujadili na uongozi.

UPENDO
1,000 TZS
kwa mwezi · 12,000/mwaka
Mwanachama1.5M
Mke/Mume1.5M
Mtoto (1-4)1M
Ulemavu (Mwanachama)1.5M
Fao la Elimu600K
FARAJA
2,000 TZS
kwa mwezi · 24,000/mwaka
Mwanachama3.5M
Mke/Mume3M
Mtoto (1-4)2M
Ulemavu (Mwanachama)3.5M
Fao la Elimu600K
TUMAINI
3,500 TZS
kwa mwezi · 42,000/mwaka
Mwanachama6M
Mke/Mume5M
Mtoto (1-4)3M
Ulemavu (Mwanachama)6M
Fao la Elimu600K
Jedwali kamili la mafao (TZS)
Aina ya Fao UPENDO FARAJA TUMAINI AMANI ⭐ Umri wa Juu
Fao la Maisha — Mwanachama 1,500,000 3,500,000 6,000,000 10,000,000 Hadi 75
Fao la Maisha — Mke/Mume 1,500,000 3,000,000 5,000,000 5,000,000 Hadi 75
Fao la Maisha — Mtoto (1–4) 1,000,000 2,000,000 3,000,000 3,000,000 Hadi 21
Ulemavu wa Kudumu — Mwanachama 1,500,000 3,500,000 6,000,000 10,000,000 Hadi 75
Ulemavu wa Kudumu — Mwenza 1,000,000 1,500,000 2,000,000 2,500,000 Hadi 75
Ulemavu wa Kudumu — Mtoto 500,000 1,000,000 1,500,000 2,000,000 Hadi 21
Fao la Elimu kwa Watoto 600,000 600,000 600,000 600,000
Bima ya Wazazi/Wakwe (Hiari) 1,000,000 – 2,000,000 TZS  ·  Ada: 9,000/mwezi (108,000/mwaka) Hadi 90
Ada ya Mwaka (mara moja) 12,000 24,000 42,000 72,000 ⭐
Utaratibu wa madai

Msiba ukitokea — hatua za kufuata:

1
Wasiliana na uongozi wa JMMBA mara moja. Wataongoza mchakato wote.
2
Kusanya hati muhimu: Fomu ya madai · Kibali cha mazishi · Kitambulisho cha marehemu · Barua ya JMMBA.
3
Wasilisha hati kwenye tawi lolote la CRDB Bank (karibu: CRDB Mbezi Beach).
4
Malipo yanafuata baada ya hati kuthibitishwa. CRDB wanasema saa 24–48, lakini kwa uzoefu wetu malipo huchukua karibu wiki moja — inategemea uharaka wa kupata hati zote kutoka kwa wafiwa na utaratibu wa benki. (Muda wa saa 48 ni wa kampuni ya bima rasmi; mazoezi halisi yanaweza kutofautiana.)
Viambatanisho vya usajili

Unahitaji nini kujiunga:

🪪
Kitambulisho — NIDA, Leseni, au Kadi ya Mpiga Kura
📋
Fomu ya Maombi ya Bima (inapatikana kwa uongozi wa JMMBA)
💳
Ada ya mwaka — 72,000 TZS (AMANI) — inalipwa mara moja
Uanachama wa JMMBA unaothibitishwa (namba yako ya JMMBA)
Kumbuka: Vikundi vya WhatsApp vinavyokuwa na uongozi vinaruhusiwa. JMMBA tayari imefika idadi inayohitajika (watu 10+) ili bima ianze.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Maswali na Majibu (FAQ)

Bima inaanza kazi mara moja baada ya malipo ya ada kukamilika. Hakuna muda wa kusubiri.
Hapana. NIDA inapendekezwa lakini Kadi ya Mpiga Kura au Leseni ya Udereva pia zinakubalika kama mbadala.
Unaweza kubadili mpango wakati wa upyaishaji wa bima tu (mwaka unaofuata). Mabadiliko hayaruhusiwi katikati ya mwaka.
Hapana. Michango haitarejeshwa kwani hutumika kusaidia wanachama wengine waliopatwa na majanga. Hii ndiyo msingi wa bima ya vikundi.
Ndiyo, kuna mpango wa hiari wa Bima ya Wazazi/Wakwe. Fao la maisha ni TZS 1,000,000–2,000,000 na ada ni 9,000/mwezi (108,000/mwaka). Kiwango cha juu cha umri ni miaka 90.
Mafao yao yatapatikana kupitia mwenza aliyepo kwenye bima. Kama wote wana zaidi ya miaka 75, watoto wao waliopo kwenye kikundi wanaweza kuwalipa kupitia mpango wa wazazi/wakwe. Masuala maalum yatathminiwa na uongozi na Kamati ya Jamii.
Hapana. Ada inalipwa mara moja kwa mwaka mzima. Hakuna malipo ya awamu.
Utaratibu wa michango ya mikeka utasitishwa rasmi mara baada ya bima ya kikundi kuanza kufanya kazi. Bima itachukua nafasi yake.
Nyaraka za Bima

Majalada ya rejea kwa wanachama

📄
Taarifa ya Kamati ya Jamii — Bima ya Vikundi 2025
Mapendekezo rasmi · Vifurushi · Jedwali la mafao · Maswali na majibu · CRDB/Sanlam
🔐
Angalia hali yako ya bima — Members Portal
Ingia kwenye akaunti yako — namba ya JMMBA au namba ya simu + nenosiri lako
Jiunge leo

Jiunga na Bima ya Faraja — kulinda familia yako.

Wasiliana na uongozi wa JMMBA au Kamati ya Jamii kupitia WhatsApp au simu. Tutakusaidia na fomu na mchakato wote wa usajili.