Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A
Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A
Hii ni sehemu maalum ya taarifa za Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A ndani ya Kata ya Kawe, Manispaa ya Kinondoni. Hapa wakazi wanaweza kuona matangazo muhimu, taarifa za utekelezaji, nyaraka za utambuzi wa wakazi, taarifa za ulinzi shirikishi, na marejeo muhimu yanayohusu maisha ya kila siku katika mtaa.
Ukurasa huu umeandaliwa ili taarifa muhimu zisiwe zinapotea kwenye vikundi au vipeperushi vya muda mfupi. Unakusanya mambo yanayohitaji kuonekana wazi, kupakuliwa kwa urahisi, na kurejelewa tena na wakazi, viongozi wa mtaa, na wadau wa maendeleo.
Tangazo muhimu
Mkutano wa wakazi kuhusu mradi wa majitaka
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A, akishirikiana na Mkandarasi wa Mradi wa Majitaka (BCEG) pamoja na DAWASA, anawakaribisha wakazi wote kwenye mkutano wa wakazi utakaofanyika Jumamosi tarehe 14/3/2026 saa 3:00 kamili asubuhi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mbezi Beach A.
Ajenda 1Kupokea taarifa ya Mradi wa Majitaka.
Ajenda 2Changamoto na kero za mradi.
Wananchi wote mnakaribishwa.
Mambo yanayopaswa kuonekana wazi
Mpango wa ulinzi shirikishi wa Mbezi Beach A
Mpango wa ulinzi shirikishi wa mtaa umegawanywa katika kanda saba: Kanda D, Kanda E, Kanda F, Ukanda wa Bahari Kaskazini, Ukanda wa Bahari Kusini, Makazi Mapya, na Capt. Komba. Idadi ya walinzi imeongezwa na itaendelea kuongezwa kulingana na mahitaji ya kiusalama yatakayojitokeza.
Barriers zitawekwa kwa awamu kulingana na mwitikio wa uchangiaji. Kwa makazi, kiwango cha uchangiaji ni TZS 20,000 kwa mwezi. Kwa maeneo ya biashara, kiwango ni kuanzia TZS 50,000 mpaka TZS 100,000 kutegemeana na aina ya biashara.
Makundi / kampuni zilizopitishwa
- Mswiha Security Company Ltd — Block D
- Muzakir Group Investment — Block E
- Nyota Security Group — Wakazi wa Block F na J
- Kikundi cha Polisi Jamii — Ukanda wa Bahari Kaskazini na Kusini
Kila mkazi anatakiwa kuweka taa kwenye fence na kufyeka vichaka vilivyo pembezoni mwa nyumba. Ukaguzi utafanyika mara kwa mara na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka maelekezo.
Malipo ya ulinzi shirikishi
CRDB: 01330003LRC01
Jina la akaunti: SERIKALI YA MTAA MBEZI BEACH A - TOZO
Malipo yafanyike kila tarehe 25–27 ya mwezi husika ili walinzi walipwe kwa wakati.
Fomu ya kutambua wakazi
Fomu hii inakusanya taarifa za mmiliki wa jengo, anayekaa, na wanakaya wote. Ikiwa nafasi haitoshi, taarifa zinaweza kuambatanishwa kwenye karatasi nyingine na kuwasilishwa ofisini au kwa WhatsApp.
WhatsApp: Simon Kivambe 0694 240210 • Ramadhani Atuman 0748 018041
Email: [email protected]
Pakua fomu ya wakazi
Kamati za Serikali ya Mtaa
Serikali ya Mtaa imeunda kamati za ulinzi, ujenzi na miundombinu, afya na mazingira, elimu na malezi, fedha na mipango, ustawi wa jamii, pamoja na michezo, burudani na utamaduni ili kusimamia majukumu ya maendeleo kwa ufanisi.
Pakua taarifa ya kamati
Mradi wa majitaka
Faili hili linaorodhesha mitaa au nyumba ambazo hazijafikiwa na mradi wa maji taka. Ni rejea muhimu kwa wakazi wanaotaka kuthibitisha hali ya eneo lao kabla ya kufuatilia kwa ofisi husika.
Pakua faili la mradi wa majitaka
Kanuni na mwongozo wa makazi
Sheria ndogo za mifugo na mwongozo wa udhibiti wa kelele na mitetemo ni nyaraka muhimu kwa makazi ya mijini. Zinasaidia wananchi kufahamu mipaka ya ufugaji, biashara ya nyama, na udhibiti wa kero za kelele.